Author: Mama Mwenyekiti

A Wife, Mother of 4 and a journalist

Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya kuangalia namna ya kuboresha mifumo ya hakijinai nchini, Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Mohamed Chande. Na Restuta James MALEZI duni, umasikini utandawazi na makundi rika, yanasababisha watoto kufanya makosa makubwa ya kijinai kama mauaji na kufanya unyang’anyi kwa kutumia silaha, ili kupata mahitaji muhimu. Meneja wa mahabusu ya Watoto jijini Dar es Salaam, Darius Damas, ameiambia Tume ya Kuangalia namna ya Kuboresha Mifumo ya Hakijiani inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Mohamed Chande, ilipotembelea mahabusu hiyo leo. Amesema mashtaka yanayowakabili watoto ni mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha, ulawiti na ubakaji, matusi, dawa za kulevya na…

Read More

Na Restuta James UWEKEZAJI uliofanywa na Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika bandari ya Dar es Salaam, umeiongezea uwezo na sasa inategemea kuhudumia zaidi ya tani milioni 20 za shehena mchanganyiko kwa mwaka. Tangu Rais Samia aiingie madarakani, ameshatoa zaidi ya Sh. bilioni 573 ili kuwekeza katika Bandari ya Dar es salaam ikiwamo ununuzi wa mitambo ya kisasa ya kupakua na kupakia makontena. Ni katika uwekezaji huo ambao umewezesha bandari nzima kufungwa kamera, ili kudhibiti wizi na kuhakikisha usalama wa shehena inayohudumiwa na bandari ya Dar es Salaam. Lengo la uwekezaji huo ni kuchochea kasi na ukuaji uchumi,…

Read More

Mwandishi Wetu na Mtandao KUNA watu ambao huwezi kukadiria umri wao licha ya kwamba wana miaka mingi, mwonekano wao unabakia kuwa wa ujana. Orodha ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), inawataja nyota kadhaa wa muziki na filamu, ambao kwa miaka mingi wamesalia kama walivyokua walipojitosa katika fani ya burudani. Kuanzia Afrika, orodha ya BBC inamtaja mwigizaji wa Nollywood nchini Nigeria, Kate Henshaw (51), ambaye mwonekano wake haufanani na miaka aliyonayo. Mashabiki wengi wa Kate walikadiria ana miaka 30, wakati aliposherehekea miaka 50 tangu kuzaliwa kwake. Kwa ufupi ni kwamba Kate Henshaw aliolewa na raia wa Uingereza, Roderick James Nuttal, mwaka wa 1999 na wakajaaliwa mtoto wa…

Read More

Na Restuta James UTAFITI wa kitabibu umeongeza matumaini katika vita dhidi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi (VVU), baada ya kuja na dawa kinga zinazoweza kumkinga mtu asiambukizwe virusi hivyo. Wataalamu wa afya wametaja dawa kinga hizo kuwa ni pete kinga inayowekwa ukeni na nyingine ni dawa ya sindano anayochomwa mtu kumkinga ndani ya miezi miwili. Akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mtendaji Mkuu taasisi isiyo ya kiserikali ya DARE Tanzania, Dk. Lilian Mwakyosi, alisema pete kinga ni miongoni mwa njia salama na rahisi kutumia ili kujikinga na VVU hususani kwa wasichana na wanawake kwa…

Read More

Na Restuta James NGULI wa nyimbo za injili nchini, Christina Shusho, amesema ‘kituo kinachofuata’ ni tamasha na maonesho ya biashara nchini Dubai, ambayo yatakwenda sambamba na mahubiri ya neno la Mungu. Shusho ameiambia GND jijini Dar es Salaam jana alipokutana na wadau wa maandalizi wa safari ya Dubai kwa wapendwa wanaomiliki biashara. Alisema safari hiyo imeandaliwa na Neema Ministry ya mtumishi wa Mungu, Nabii Neema Sikatenda, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alisema safari ya Dubai inajumuisha matukio matano ambayo ni mikutano ya kibiashara, mikutano ya injili, onesho la muziki wa injili, utalii na maonesho ya kibiashara. “Ni tukio muhimu…

Read More