Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- BRELA, UDSM wawanoa wadau faida miliki ubunifu
- Utafiti kilimo, mifugo na uvuvi kutokomeza njaa
- NMB yaja na mwarobaini mikopo kausha damu
- TARI kuzalisha miche 100,000 ya parachichi msimu ujao
- BBT YAANZA KUZAA MATUNDA KWENYE UVUVI
- MAREKANI YATOA BIL 60/- KUIMARISHA USALAMA WA CHAKULA
- BOT YAONYA APP ZA MIKOPO MTANDAONI, YAPIGA MARUFUKU UDHALILISHAJI
- VIJANA, WANAWAKE WAPEWA MITAJI WEZESHI MILIONI 101/-
Author: Mama Mwenyekiti
TAASISI ya Saratani Ocean Road (ORCI), imetenga siku maalumu ya uchunguzi wa saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino. Taarifa ya ORCI iliyotolewa leo imesema kwamba taasisi hiyo imetenga saa saba kila siku ya Alhamisi kuhudumia kundi hilo la wagonjwa. “Kliniki ya saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino kila Alhamisi kuanzia saa 2:00 hadi saa 9:00 alasiri block A-chumba namba 110,” imesema. Taarifa hiyo imeongeza kuwa: “Karibu upate elimu na uchunguzi wa awali wa saratani…karibuni hata kwa watu wengine wa kawaida.”
MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), imeita wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda ili waendeleze maeneo saba yaliyopo katika mikoa ya Mbeya, Lindi, Dar es Salaam, Tanga na Shinyanga, chini ya utaratibu wa mamlaka hiyo. Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Charles Itembe, kwa vyombo vya habari imeyataja maeneo yaliyopo Dar es Salaam kuwa ni vitalu namba 184/185 na 186/185 vyenye jumla ya ekari 8.39, zilizopo eneo la viwanda Chang’ombe, katika Manispaa ya Temeke, zilizokuwa zinamilikiwa na iliyokuwa kampuni ya taifa ya chuma. Lingine kwa Dar es Salaam ni mita za mraba 15,000 zilizopo eneo Maalum la Kiuchumi…
SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Mkoa wa Dar es Salaam, limekuja na mkakati wa kusaidia wajasiriamali wadogo kumiliki viwanda baada ya kujenga kituo cha kisasa cha kusindika mazao ya kilimo, chenye huduma muhimu za viwanda vidogo. Meneja wa SIDO, Mkoa wa Dar es Salaam, Ridhiwani Matenge, amesema kituo hicho kinajengwa kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea (KOIKA) na kipo mbioni kukamilika. “Ni kituo ambacho kitaweza kutoa mafunzo na uzalishaji kwa wakati mmoja ambapo wajasiriamali watapata mafunzo kwa vitendo na pia itakuwa ni sehemu ya kuzalishia. Jengo hilo likikamilika na kuwekwa vitendea kazi, litakuwa na maeneo sita ya…
TAASISI ya Afya Ifakara (IHI), imeanza kampeni kubwa ya chanjo ya mbwa ili kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Kampeni hiyo inafanyika kwa siku 10, kuanzia Jumamosi iliyopita hadi kesho Jumatano. Akizungumza na NIPASHE, kiongozi wa kampeni hiyo kutoka IHI, Dk. Sambo Maganga, amesema kampeni hiyo inafanyika Manispaa ya Tabora Mjini na wanatarajia kuchanja mbwa 15,000 ili kudhibiti ugonjwa huo katika eneo hilo. Kwa mujibu wa taasisi hiyo, ugonjwa wa kichaa cha mbwa husababisha vifo vya watu 552 nchini kwa mwaka huku asilimia 98 waking’atwa na mbwa wa kufugwa.
UGONJWA wa saratani umeendelea kuwa tishio kwa wanawake kutokana na sababu kadhaa ikiwamo kutonyonyesha ipasavyo, kuchelewa kupata mtoto na kutopata chanjo kwa wakati. Takwimu za Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), za Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu, zinaonyesha kwamba, Tanzania inapata wagonjwa wapya 42,046 kila mwaka na miongoni mwao ni asilimia 44 ya wanawake wanaokabiliwa na saratani ya mlango wa kizazi. Mkurugenzi Mkuu wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage, anasema saratani ya shingo ya kizazi ni tatizo kubwa na imeendelea kuongezeka siku hadi siku. Anasema wanawake walio kwenye hatari ya kupata aina hiyo ya saratani ni wale wenye…
Na Restuta James WANASAYANSI wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI), wanajifungia maabara kwa mwaka mmoja, kutafiti sababu za kuenea kwa ugonjwa sugu wa figo (CKD) na hatari inayowakabili wagonjwa wa tatizo hilo, katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Utafiti huo uliopewa jina la RenalTWO ni uchunguzi wa kwanza wa muda mrefu juu ya magonjwa sugu ya figo (CKD), ambao umeanza Aprili Mosi, mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Machi 31, mwakani. Taarifa iliyotolewa na IHI kwenye tovuti yake, ilieleza kuwa utafiti huo utachunguza matukio ya kuenea kwa CKD, kisukari na shinikizo la damu.
DAKIKA mbili na sekunde 14 tangu walipoanza kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki, watoto wa ‘mtaani’ kutoka jiji la Kampala Uganda, zilitosha kumnyanyua jaji Bruno Tonioli, ambaye aliwapa alama ya dhahabu kwa burudani waliyokuwa wanaitoa. Hawa si wengine bali ni kundi la Ghetto Kids, linalolelewa na mwalimu Dauda Kavuma, ambaye anawachukua kutoka mitaani wengine wakiwa yatima au kukosa malezi; na hivyo kuwapa malezi pamoja na huduma zote muhimu. Watoto hawa wamefanikiwa wateka mioyo ya takribani mashabiki 2,286 waliokuwa wanafuatilia onyesho la vipaji la Britain Got Talent, wakati wa kurekodiwa katika ukumbi wa Palladium, jijini London, nchini Uingereza wiki mbili zilizopita.…
DODOMA, Tanzania WAKATI watu wengi wakitazama njiwa kama kitoweo na mapambo, ndege huyo anaweza kufugwa kibiashara na kuiingizia familia kipato cha kutosha. Deogratius Temba, kijana kutoka Dodoma, Tanzania anafuga njiwa wa kipekee na wanamuingizia kipato cha kutosha. Njiwa anaofuga Temba maarufu kama Manjiwa hutumika kupendezesha makazi, maofisi ama sehemu zingine kama mahoteli na za kupumzikia. Kati zaidi ya aina 10 ya njiwa wa mapambo alionao Deogratius, mmoja anauzwa kati ya dola $85 mpaka $180 au Sh. 400,000. Unaweza kujiuliza wanafananaje njiwa hawa, na kwanini kijana huyu maarufu kama Deo Manjiwa ameamua kuwafuga njiwa hawa wa mapambo? Mwandishi wetu Yusuph Mazimu…
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. WAFUGAJI kote nchini wametakiwa kutenga maeneo ya malisho katika msimu huu wa mvua kwa ajili ya matumizi wakati wa kiangazi, ili kuepuka migogoro baina yao na wakulima. Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia wizi wa Mifugo nchini, ACP Simon Pasua, aliyasema hayo jana wilayani Monduli, alipokutana na viongozi wa wafugaji pamoja na wakulima, kwa lengo la kupanga mikakati ya pamoja ya kuepusha migogoro ambayo imekua ikijitokeza wakati wa kiangazi. Kamanda Pasua alibainisha kuwa wakati wa kiangazi kunakuwa na ukame hivyo kukosekana sehemu za malisho, hali ambayo inasababisha baadhi ya wafugaji kupeleka mifugo sehemu ambazo…
Mwonekano wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere Na Restuta James MIEZI minne baada ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuzindua ujazaji wa maji katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP), katika Mto Rufiji, mkoani Pwani, ujenzi wake umebakisha asilimia 14.4 pekee kukamilika. Bwawa hilo linalotazamiwa kuzalisha megawati 2,115 za umeme litakapokamilika, limebakisha ujazo wa maji futi 10.53 pekee, kuanza uzalishaji wa awali. Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewaambia waandishi wa habari leo kwamba ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 85.6. “Bwawa letu la Mwalimu Nyerere ni moja ya miradi ambayo inakwenda vizuri na utekelezaji unaendelea…mwakani Juni tunataka…