Author: Mama Mwenyekiti

A Wife, Mother of 4 and a journalist

MOJA kati ya malengo ya endelevu ya dunia ni kuhakikisha kwamba hadi kufikia mwaka 2033, asilimia 80 ya kaya ziwe zinatumia nishati safi ya kupikia. Lengo hili linakuja na mageuzi ya kiteknolojia ya uvumbuzi wa majiko yanayotumia nishati kidogo kwa ajili ya kupikia na kuhakikisha upatikanaji wake kwa gharama nafuu ili watu wa kada zote mijini na vijijini, waweze kuzipata. Majiko yanayotajwa hapa ni yale yanayotumia kuni, mkaa, mafuta ya kupikia (bioethanol), gesi na umeme kidogo. Kutokana na umuhimu wa nishati hasa kwa ajili ya kupikia, Umoja wa Ulaya (EU), nchini umetenga EURO milioni 17 (takribani Sh. bilioni 47.6), kwa…

Read More

UPATIKANAJI wa uhakika wa gesi, mafuta maalumu ya kupikia (bioethanol), mkaa na kuni mbadala ndilo suluhisho la uharibifu wa mazingira na kupunguza athari za mbadiliko ya tabia nchi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji ya Maendeleo (UNCDF), limesema. Ofisa Mwandamizi wa masuala ya fedha wa UNCDF na Meneja wa mradi wa Cookfund, Imanuel Muro, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi alipokuwa akizindua kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ya ‘Anzia Jikoni-mabadiliko ya hewa safi ya baadae yanaanzia jikoni.’ Alisema ili kuwezesha upatikanaji wa nishati safi, Umoja wa Ulaya (EU), umetenga EURO milioni 17…

Read More

KIOO ni moja ya pambo la ndani lenye ‘ladha’ ya kipekee kutokana na nguvu yake ya kubadili mwonekano wa chumba au eneo kwa ujumla. Wataalamu wa mapambo ya ndani wanaeleza kuwa kioo ni pambo ambalo limetumika kwa karne kadhaa bila kuchuja thamani yake. Moja ya sifa ya kipekee ya kutumia kioo kama pambo ni uwezo wake wa kubadili mwonekano wa chumba kidogo kuwa kikubwa na kupunguza eneo kubwa kuwa la kawaida, kulingana na namna ya uwekaji. Akizungumza na GND mapema leo Juni 9, 2023, mtaalamu wa mapambo ya ndani, Winnie Joseph, anasema kioo ni pambo linalowekwa sehemu tofauti tofauti kuanzia…

Read More

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema visiwa hivyo vina nafasi ya kuendelea kushirikiana na Serikali ya Ujerumani kwenye uwekezaji katika sekta ya utalii. Ameyasema hayo leo Juni 8, 2023 alipozungumza na Balozi wa Ujerumani, Regine Hess, ambaye amemaliza muda wa utumishi wake nchini Tanzania. Rais Mwinyi amesema Ujerumani imetoa mchango mkubwa visiwani hapa kupitia sekta ya majisafi na salama, ambayo aliieleza kuwa muhimu kwa ustawi wa wananchi wa Zanzibar. Ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano wanaoutoa kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia sekta za afya na michezo, pamoja na kushajihisha watalii raia wa nchi hiyo, kutembelea vivutio vya…

Read More

SEHEMU ya kulia chakula ni moja ya eneo muhimu ndani ya nyumba yoyote na ndio maana mtu anapojenga nyumba anazingatia eneo hili. Mtaalamu wa mapambo ya ndani, Simon Alex, anaeleza kuwa mabadiliko makubwa yanayoendelea kwenye sekta nyingine yameigusa pia sekta ya nyumba na mazingira kwa ujumla, akizungumzia eneo la chakula. Akizungumza GND anasema chakula hakipaswi kuwekwa kwenye meza ya chakula watu wanapokaa na kula. Badala yake, anasema meza ya bufee ndio inayopaswa kuwekwa chakula na inatakiwa iwekwe pembezoni mwa meza ya chakula ili iwe rahisi kwa mtu anapopakua chakula kufika mezani kula. Anasema meza hiyo inapaswa kuwa ndefu kiasi na…

Read More

SERIKALI ya Norway imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kupitia Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), katika miradi mbalimbali ukiwamo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Balozi wa Norway nchini, Elisabeth Jacobsen, ameyasema hayo alipotembelea SUA na kuona miradi ya ushiriki wa vijana kwenye kilimo. Amesema kwa zaidi ya miaka 50, Tanzania na Norway zimekuwa na uhusiano mzuri hivyo anakusudia kuendeleza ushirikiano huo kwa kuanzisha na kuendeleza miradi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi hususani hewa ukaa. “Norway pia kuna mambo mengi ya kushirikiana… hatutashiriki kwenye kilimo pekee bali hata kwenye masuala ya miradi ya mabadiliko ya hali ya hewa,” amesema…

Read More

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Ikulu mjini Unguja mapema leo. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Charles Hillary, kwa vyombo vya habari imesema kwamba viongozi hao wamezungumzia ustawi wa Zanzibar kisiasa na kijamii. “Viongozi hao wameafikiana kwamba ipangwe tarehe ya kuzindua rasmi kamati maalumu itakayoundwa na wajumbe kutoka CCM (Chama Cha Mapinduzi) na ACT-Wazalendo, ambavyo ndivyo vilivyounda serikali ya Umoja wa Kitaifa, kuanza kujadiliana na baadae kupanga mpango wa utekelezaji wa ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa,” imesema sehemu ya taarifa hiyo. Imefafanua kuwa viongozi wa…

Read More

Benki ya NBC imetoa gawio la Sh. bilioni sita kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana mwaka 2022. Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya hundi iliyofanyika leo Mei 17, Jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, ameipongeza NBC ambayo Serikali ni mmoja ya wanahisa, ikimiliki asilimia 30 ya hisa zake, amesema mafanikio hayo ni matokeo chanya ya utendaji mzuri uliowezesha kupatikana kwa faida nzuri. “Serikali inafurahi kuona uwekezaji wake unakuwa wenye tija. Kiasi cha shilingi bilioni sita tulichopokea leo, kitasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,” amesema Mchechu. Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Elirehema…

Read More