Author: Mama Mwenyekiti

A Wife, Mother of 4 and a journalist

Na Restuta James MKOA wa Kagera unatarajiwa kuunganishwa kwenye gridi ya taifa baada ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kusaini mkataba wa kusimamia ujenzi wa vituo vya kupoza na kusafirisha umeme wa kilovoti 220. Mradi huo utagharimu dola za Marekani milioni 135.4 na utasimamiwa na kampuni ya Shaker Consultancy ya Misri ambayo ni mhandisi mshauri kwa kushirikiana na kampuni ya usimamizi wa miradi ya umeme ya Saudi Arabia (PDC). Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 13, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Gissima Nyamo-hanga, amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa kituo…

Read More

Na Restuta James KAMA huna fedha za kutosha na unahitaji jiko la nje wala usiwaze tena. Kuna njia za kuwa na sehemu ya kupikia yenye hadhi nzuri na mandhari ya kuvutia na kuifanya nyumba yako kuwa ya kisasa kila wakati. Mtaalamu wa bustani, Georgia Lindsay, ameandika kwenye mtandao wa Houzz kuwa jiko la nje linaweza kuwekwa kwenye eneo la bustani kwa kuweka karo la kuoshea vyombo, vyakula na jiko lenyewe. Hii ni aina ya ubunifu ambao unawapa nafasi wenye nyumba kufurahia mazingira ya nje badala ya kila siku kutumia ndani pekee. Katika eneo hili la jiko, wanafamilia wanaweza kufurahia mlo…

Read More

Na Restuta James MWISHONI wa juma yaani Jumapili kulikuwa na vibe la aina yake baada ya kuhitimisha msimu wa ligi kuu ya Uingereza kwenye mchuano mkali kati ya klabu za Arsenal na Manchester City, zilizokuwa zikiwania taji la EPL lililotwaliwa na wenyeji wa Etihad waliochukua ‘ndoo’ kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya washika bunduki, Arsenal. Ni hitimisho la aina yake hasa kutokana na kwamba mshindi wa taji alitarajiwa kutangazwa katika mechi ya 38 ya kufunga msimu; hivyo lilikumbwa na msongo wa kila aina. Katika mazingira hayo, ni vizuri ukawa na vitu vya kuimarisha afya yako kujiondoa kwenye msongo wa…

Read More

Na Restuta James KWA wapenda maua neno hydroponics haliwezi kuwa geni kwao kwa kuwa ni lugha ya mkitaalamu kwa mimea inayokua ndani ya maji pasipokuweka udogo. Upandaji huu wa maua ni mzuri hasa kwa ‘walevi’ wa mimea kwani ni rahisi kuiweka popote ikiwamo jikoni, chumbani au chooni (kwa maua yanayosafisha hewa). Upandaji huu wa mimea au maua haya una ‘ladha’ ya pekee ndani ya nyumba kutokana na kwamba yanatumia zaidi majagi ya udongo. Wataalam wa bustani wanaeleza kuwa upandaji huu unavutia na kuongeza ‘usafi’ ndani ya nyumba kwa kuwa ua na chombo vyote ni lazima viwe visafi wakati wote. Wanaeleza…

Read More

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wamesaini makubaliano na Taasisi nne za Serikali ya kushirikiana ili kuleta ufanisi katika maeneo mbalimbali ya kibiashara. BRELA na Chuo Kikuu Mzumbe, TIA na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viutilifu Tanzania (TPHPA), wamesaini makubaliano hayo, leo Mei 9, 2024 kwenye maadhimisho ya siku ya Miliki Ubunifu jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji, ameiagiza BRELA na COSOTA kutoa elimu zaidi kwa wabunifu nchini ili wanufuike na kazi zao na kuhakikisha inatambulika,…

Read More

Na Mwandishi Wetu MILANGO imefunguliwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kunufaika na mafunzo ya umahiri katika nchi za Ulaya na Marekani, kupitia programu ya kimataifa ya mafunzo kazini. Aidha, wanafunzi waliopo katika vyuo vya kati vinavyotoa stashahada (diploma), ya kilimo na mifugo wanapewa nafasi hiyo, inayotolewa na Chama cha Ushirika cha Wajasiriamali Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUGECO). Akizungumza kwenye mjadala wa Jiajiri uliofayika SUA, Mkurugenzi Mkuu wa SUGECO, Revocatus Kimario, amesema fursa hiyo inawahusu wanafunzi kuanzia mwaka wa pili wanaosoma kozi za sayansi ya mifugo, ranchi, dawa za mifugo, ufugaji, afya ya mifugo na kilimo kwa…

Read More

Na Restuta James CHUO cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kimeanzisha utafiti kwa ajili ya kutambua mchango wa wanawake mashujaa wa Tanzania walioshiriki harakati mbalimbali za kuijenga nchi kuanzia za kupinga ukoloni na kudai uhuru. Akizungumza na jijini Dar es Salaam na BUSTANI, Mkuu wa Idara ya Stadi za Jinsia katika chuoni hapo, Dk. Sarah Mwakyambiki, amesema utafiti huo ulianza miaka minne iliyopita na tayari wamewatambua wanawake 63, ambao mchango wao katika harakati za ujenzi wa taifa haujatambuliwa ipasavyo. “Shujaa kwa mantiki ya ni mwanamke wa kwanza kufanya jambo fulani nchini; tumewatazama ambao kwa kiasi kikubwa walifanyakazi na Mwalimu Nyerere. Utafiti…

Read More

Na Restuta James NI simulizi ya kusisimia ya msichana mwenye miaka 28, ambaye ni yatima asiyewafahamu baba na mama yake mzazi, aliyepewa msaada wa cherehani na Rais Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni. Si mwingine bali ni Beatrice Mwalingo, ambaye ujumbe wake wa maneno 10 umefanikisha kumtambulisha kwa Mkuu wa Nchi, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwenye dunia ya ushonaji, wateja na kuongeza ajira kwa vijana. Historia ya msichana huyo imebebwa kwa kiasi kikubwa na mageuzi ya teknolojia kuanzia kujifunza kwake kushona hadi kukutana na msaada wa Rais Samia. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Beatrice anasema baba yake alikuwa ni…

Read More

“Tiba shufaa ni maalumu kwa ajili ya kuimarisha maisha ya mgonjwa, kimwili, kiakili na kiroho ili aweze kuishi vizuri wakati wote wa kuugua,” anasema. Na Restuta James UKIKUTANA naye huwezi kudhania kwamba ni mtu mwenye changamoto ya maradhi. Sura yake yenye nuru na ukaribisho wa tabasamu ni vitu vitakavyokuhakikishia kuwa Jasmin Said Salum ni mwanamke mwenye maisha ya kawaida kama wengine. Jasmin shujaa wa saratani mwenye miaka 33, alibainika kuwa na maradhi hayo miaka mitatu iliyopita na kukatwa titi moja. Akizungumzia safari yake ya ugonjwa hadi kuwa shujaa, Jasmin anasema siku moja aliona ana uvimbe kama gololi kifuani ambao…

Read More

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la saba la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi ambalo litafanyika Jijini Dodoma Septemba 29, mwaka huu, likiwa na kaulimbiu ya ‘Uwezeshaji wa Uchumi Endelevu’. Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, amewaambia waandishi wa habari Jijini hapa jana kuwa kongamano hilo litatanguliwa na wiki ya uwezeshaji sambamba na maonesho ya siku tatu ya wajasiriamali yatakayoanza tarehe 26 hadi 28, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete. “Maenesho hayo ya siku tatu kabla ya kongamano yana maana kubwa katika dhana nzima ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwani wajasiriamali…

Read More