Author: Mama Mwenyekiti

A Wife, Mother of 4 and a journalist

WANANCHI 75,000 wamefikiwa na programu ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA), katika mikoa nane, wengi wao wakiwa ni wanawake na vijana. Akizungumza na BUSTANI jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, amesema lengo la mpango huo ni kuimarisha uchumi wa vijana, wanawake, watu wenye ulemavu pamoja na wazee, ambao tayari wanafanya biashara ndogo ndogo kwenye vikundi au mmoja mmoja.

Read More

Na Mwandishi Wetu, Morogoro WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), umetahadharisha matumizi ya ‘vishoka’ kusajili kampuni, huduma au majina ya biashara, kwa kuwa wengi hutumia taarifa za wahusika vibaya. Akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya waandishi wa habari za biashara yanayofanyika mjini hapa, Meneja katika sehemu ya makampuni BRELA, Lameck Nyangi, amesema huduma za taasisi hiyo zinapatikana kwa urahisi kwa njia ya mtandao (ORS), ambao unamlazimu mhusika kujisajili kwa jina lake ili aweze kuhudumiwa. “Unakuta mtu anarahisisha tu mambo, anamtafuta mtu anamwambia amsajilie kampuni hadi anampa taarifa zake muhimu wala hajishughulishi kujua ni namna gani mfumo unafanyakazi, matokeo yake…

Read More

Na Restuta James FAMILIA nyingi kama sio zote zenye uwezo wa kununua televisheni au radio wanazo. Nyumba hizo hizo, ni chache au chini ya nusu hazina maktaba walau ya vitabu vichache. Hali hii imejenga tabia ya wanafamilia na hasa watoto kupenda kuangalia na kusikiliza vipindi zaidi badala ya kusoma. Kama wewe ni mzazi au mlezi nakuletea mbinu ya kuanzisha maktaba ndogo nyumbani ili watoto wanufaike na maarifa mengi yaliyofichwa vitabuni. Walimu wa watoto wadogo wanaeleza kuwa mtoto mwenye umri kuanzia miaka miwili na nusu wanauwezo wa kujifunza kusoma na wakajua ndani ya muda mfupi, kama mazingira wenzeshi wataanzia nyumbani. Wanashauri…

Read More

Na Restuta James UKISASA wa vitu vingi duniani unahamia kwenye kuboresha vitu vya asili kuanzia aina ya ujenzi wa nyumba hadi mapambo yake. Leo tunaangazia mapambo ya ndani yanayotokana na vitu asilia kama ukili, katani, migomba na kamba za aina mbalimbali ambazo miongo kadhaa iliyopita zilionekana kama vitu vya watu masikini. Kama inavyoonekana pichani, ubunifu wa kazi za mikono zilizonakishiwa kwa rangi ni pambo la nyumba za ‘matajiri’ ndani na nje ya Afrika. Wataalamu wa mapambo ya ndani wanaeleza kuwa sanaa ya ubunifu ndio inaosababisha kazi za mikono kuteka soko la kimataifa la urembo na mapambo. Anastazia Jonathan, anasema upambaji…

Read More

Na Mwandishi Wetu, Morogoro WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), umesema matumizi ya teknlojia kupata huduma zinazotolewa na taasisi hiyo yameondoa urasimu na kuwawezesha wananchi kupata leseni katika kipindi cha siku moja hadi tatu za kazi. Akizungumza kwenye mafunzo ya waandishi wa habari mjini hapa leo Juni 18, 2024; Mkurugenzi wa Leseni BRELA, Andrew Mkapa, amesema maboresho ya wakala huo ambayo yamewaruhudu wafanyabiashara kujisajili kwa mfumo wa mtandao (online), yanalenga kupunguza muda wa kupata huduma hadi siku moja. “Tunataka kama mfanyabiashara atakuwa amekamilisha vielelezo vyote muhimu kama namba ya mtambulisho wa mlipa kodi, kitambulisho cha taifa, vibali vya…

Read More

Na Restuta James, Morogoro KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdalllah, amewahimiza waandishi wa habari kuelimisha umma umuhimu wa kurasimisha biashara, ili waweze kunufaika na fursa zitakazowawezesha kukuza mapato. Dk. Hashil ameyasema hayo leo Juni 18, 2024, mjini Morogoro alipokuwa akifungua mafunzo ya waandishi wa habari wanaoripoti kutoka jiji la Dar es Salaam. Amesema kupitia vyombo vya habari, umma unaweza kupata taarifa muhimu kwa haraka na kwa wakati, ikiwemo namna ambavyo wananchi wanaweza kutumia mabadiliko na ukuaji wa teknolojia, kurasimisha biashara kupitia kwa Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA). “Niwaombe ndugu zangu wanahabari, kupitia…

Read More

Na Restuta James MKOA wa Kagera unatarajiwa kuunganishwa kwenye gridi ya taifa baada ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kusaini mkataba wa kusimamia ujenzi wa vituo vya kupoza na kusafirisha umeme wa kilovoti 220. Mradi huo utagharimu dola za Marekani milioni 135.4 na utasimamiwa na kampuni ya Shaker Consultancy ya Misri ambayo ni mhandisi mshauri kwa kushirikiana na kampuni ya usimamizi wa miradi ya umeme ya Saudi Arabia (PDC). Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 13, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Gissima Nyamo-hanga, amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa kituo…

Read More

Na Restuta James KAMA huna fedha za kutosha na unahitaji jiko la nje wala usiwaze tena. Kuna njia za kuwa na sehemu ya kupikia yenye hadhi nzuri na mandhari ya kuvutia na kuifanya nyumba yako kuwa ya kisasa kila wakati. Mtaalamu wa bustani, Georgia Lindsay, ameandika kwenye mtandao wa Houzz kuwa jiko la nje linaweza kuwekwa kwenye eneo la bustani kwa kuweka karo la kuoshea vyombo, vyakula na jiko lenyewe. Hii ni aina ya ubunifu ambao unawapa nafasi wenye nyumba kufurahia mazingira ya nje badala ya kila siku kutumia ndani pekee. Katika eneo hili la jiko, wanafamilia wanaweza kufurahia mlo…

Read More

Na Restuta James MWISHONI wa juma yaani Jumapili kulikuwa na vibe la aina yake baada ya kuhitimisha msimu wa ligi kuu ya Uingereza kwenye mchuano mkali kati ya klabu za Arsenal na Manchester City, zilizokuwa zikiwania taji la EPL lililotwaliwa na wenyeji wa Etihad waliochukua ‘ndoo’ kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya washika bunduki, Arsenal. Ni hitimisho la aina yake hasa kutokana na kwamba mshindi wa taji alitarajiwa kutangazwa katika mechi ya 38 ya kufunga msimu; hivyo lilikumbwa na msongo wa kila aina. Katika mazingira hayo, ni vizuri ukawa na vitu vya kuimarisha afya yako kujiondoa kwenye msongo wa…

Read More

Na Restuta James KWA wapenda maua neno hydroponics haliwezi kuwa geni kwao kwa kuwa ni lugha ya mkitaalamu kwa mimea inayokua ndani ya maji pasipokuweka udogo. Upandaji huu wa maua ni mzuri hasa kwa ‘walevi’ wa mimea kwani ni rahisi kuiweka popote ikiwamo jikoni, chumbani au chooni (kwa maua yanayosafisha hewa). Upandaji huu wa mimea au maua haya una ‘ladha’ ya pekee ndani ya nyumba kutokana na kwamba yanatumia zaidi majagi ya udongo. Wataalam wa bustani wanaeleza kuwa upandaji huu unavutia na kuongeza ‘usafi’ ndani ya nyumba kwa kuwa ua na chombo vyote ni lazima viwe visafi wakati wote. Wanaeleza…

Read More