Author: Mama Mwenyekiti

A Wife, Mother of 4 and a journalist

Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo, amewataka wabunifu wote nchini kulinda bunifu zao kwa kuzisajili kisheria, ili zisichukuliwe na watu wengine na kujinufaisha nazo bila kufuata utaratibu wa kisheria. Ametoa wito huo wakati wa ziara aliyoifanya ofisi za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), jijini Dar es Salaam ili kujionea utendaji kazi na kujifunza namna wakala inavyotoa huduma. Amesema kuna bunifu nyingi ambazo zinachukuliwa na watu wengine wanaziendeleza na kujiongezea kipato, bila wabunifu waanzilishi kunufaika na chochote kwa kuwa hawakuzisajili. “Ninatoa wito kwa Watanzania wabunifu wote kusajili bunifu zenu kupitia BRELA, maana taasisi hii inakazi ya kulinda…

Read More

VIJANA 10 wa Kitanzania wameula kwa kupata ufadhili wa Sh. 250 milioni, kutoka Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Umoja wa Ulaya (EU) na Ubalozi wa Ireland, ili kuendeleza bunifu zao zinazolenga kuboresha upatikanaji wa nishati safi nchini. Wabunifu hao 10 ni sehemu ya 159 waliowasilisha mawazo bunifu na kufanyiwa mchujo na wataalamu wa masuala ya nishati. Naibu Kamishna wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Imani Mruma, amesema lengo la kuanzishwa mchakato wa kufadili bunifu kwenye nishati ni kuchochea maendeleo ya suluhisho na teknolojia za msingi zenye uwezo wa…

Read More

Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Mwajuma Hamza, amewataka wanawake na vijana kuchangamkia fursa ya Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), ili wakuze haraka biashara zao. Ameyasema hayo mkoani Kagera alipokuwa akifungua mafunzo ya taratibu, kanuni na sheria za kufanya biashara katika eneo hilo, yaliyoandaliwa na TWCC kwa kushirikiana na Trade Mark Africa. Alisema soko hilo linakadiriwa kuwa na watu bilioni 1.3 na kwamba programu nyingine inayotekelezwa na chemba hiyo ni ile ya zabuni (Bid for Success-B4S). “Kiu yetu ni kuona wanawake na vijana wanafika masoko makubwa, wanapata zabuni za serikali na binafsi na kwenye miradi…

Read More

WANAWAKE na vijana wameanza kupigwa msasa ili waweze kushiriki zabuni za umma na binafsi, kwa kupewa mbinu za kuandaa nyaraka zinazokidhi taratibu za kisheria wakati wa mchakato wa kuomba kazi au kutoa huduma kwenye taasisi mbalimbali. Wanawake na vijana 30 wameanza mafunzo hayo katika awamu ya kwanza jijini Dar es Salaam na yanatolewa na Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), kwa ufadhili wa TradeMark Africa. Akifungua mafunzo hayo leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC, Mwajuma Hamza, amesema: “Tunategemea kuwafikia takribani wanawake na vijana 400 ndani ya miaka mitatu na katika kundi la kwanza tumeanza na 30. Watejengewa uelewa wa kina kuhusu…

Read More

Kampuni ya PASS Trust kwa kushirikiana na Benki ya Equity Tanzania wameingia mkataba wa kuwawezesha wajasiriamali walio kwenye mnyororo wa kuongeza thamani mazao ya kilimo, ufugaji, uvuvi, mazao ya misitu na viwanda. Wamesaini mkataba wa kuendeleza uhusiano wa kibiashara mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde na kuratibiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa PASS Trust, Adam Kamanda pamoja na Meneja Mkuu wa Biashara wa Equity Benki, Leah Ayoub katika Maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi (Nane Nane – 2024) yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane jijini Dodoma. Mkataba uliosainiwa unalenga kuwafikia zaidi wakulima wadogo na wa kati…

Read More

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema itaendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa wakulima ili waweze kupata mikopo kwa riba nafuu itakayowasaidia kufikia malengo na kupiga hatua ya maendeleo. Akizungumza kwenye mahojiano katika Maonesho ya kimataifa ya kilimo Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma, Afisa Mkuu Mwandamizi, Kurugenzi ya Usimamizi Sekta ya Fedha, Idara ya huduma ndogo ya Fedha, BoT, Deogratius Mnyamani, amesema BoT imetenga fedha kwa ajili ya taasisi za fedha zikiwamo benki ili waweze kuwakopesha wakuilimo kwa riba nafuu. Amesema lengo ni kuhakikisha wakulima wanapata mikopo kwa gharama nafuu ili kuleta tija kwa Taifa katika sekta ya kilimo. Amesema ili mkulima…

Read More

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imejipanga kuwasaidia Wajasiriamali nchini kupitia Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi (ECGS), pamoja Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SME-CGS). Lengo ni kuwezesha wakopaji wenye miradi mizuri, kupata mitaji kutoka kwenye benki na taasisi za fedha, pale wanapokuwa na upungufu wa dhamana ambayo inatoa fursa ya udhamini. Akizungumza katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Fedha wa BoT, Gloria Samwel Chellunga, amesema benki hiyo inasimamia mfuko wa udhamini wa mkopo kwa niaba ya serikali ili…

Read More

Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), imewataka Watanzania kuchangamkia uwekezaji katika maeneo hayo ili wazalishe bidhaa zinazokidhi soko la nje ili kuiongezea nchi fedha za kigeni. Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa uhamasishaji wa EPZA, Nakadongo Phares, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane-nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma. “Tuko hapa Nane-nane kutoa elimu kwa wananchi, lakini pia kuelezea fursa zilizopo za kupata maeneo maalum katika fursa za uwekezaji wa viwanda vinavyozalisha kwa ajili ya kuuza nje ya nchi,” amesema Nakadongo. Amesema EPZA ina programu ya kumwezesha…

Read More

Na Mwandishi Wetu Vijana wanaopenda kujiunga na mafunzo ya ufundi wa fani mbalimbali wameitwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kujiunga na vyuo vyake vilivyopo mikoa yote nchini. Tangazo la VETA limetaja baadhi ya fani za ufundi zinaotolewa ni umeme wa magari (AE), mitambo, majokofu na kiyoyozi, ufungaji umeme, msaidizi wa maabara, Sekretarieti na kompyuta, useremala na uunganishaji, teknolojia ya ushonaji na ubunifu wa mavazi na uashi na ufyatuaji matofali. Nyingine ni ujenzi na matengenezo ya barabara, uchoraji na uandishi wa alama, uchomeleaji na utengenezaji wa vyuma, teknolojia ya usindikaji wa nyama, mapishi, huduma za chakula…

Read More

WANAWAKE, Vijana na wenye mahitaji maalumu wameshauriwa kujiunga na mfumo wa manunuzi ya umma (National e-Procurement System of Tanzania-NeST), ili waweze kuona zabuni za umma mara tu zinapotangazwa na kuziomba. Akizungumza kwenye mkutano wa asubuhi (breakfast meeting), ulioandaliwa na Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), na kuwakutanisha wanawake na vijana zaidi ya 300, Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Kanda ya Pwani, Vicky Mollel, amesema wanawake wana nafasi ya kukuza biashara zao kupitia miradi ya serikali kwa njia ya zabuni. Amesema ili kushinda zabuni, ni muhimu kwa wanawake kujisajili kwenye mfumo wa NeST, ili watambulike na…

Read More