Author: Mama Mwenyekiti

A Wife, Mother of 4 and a journalist

Na Mwandishi Wetu WOTE tunakubali kwamba mimea na maua kwa ujumla, inafanya mandhari ya nyumba iwe nzuri na ya kuvutia. Hata hivyo, usalama wa watu na wanyama wanaofugwa unapaswa kupewa uzito unaostahili pindi mtu anapopanga kutengeneza bustani. Hii ni kwa sababu yapo maua yanayovutia kwa mwonekano pindi yanapochanua, lakini yanaweza kusababisha hasara ya muda mrefu ikiwamo kuharibu ardhi hadi kusababisha kifo kwa watu na wanyama. Mimea hii inatajwa kuwa na kiwango kikubwa cha kemikali zenye sumu zinazoweza kusababisha shida ya tumbo, matatizo ya kupumua na maradhi ya moyo. Mtaalamu wa bustani, Luciana Massawe, anasema hatua ya kwanza ya kuchukua ni…

Read More

Na Mwandishi Wetu UNASUMBULIWA na nyoka au wadudu wakali? Je, nyumba yako iko kwenye mazingira ambayo nyoka anaweza kuingia? Usigope. Ipo mimea ambayo inaweza kuwafukuzia mbali na kukuhakikishia usalama. Licha ya kwamba baadhi ya mimea inastawi vizuri zaidi kwenye maeneo ya baridi, lakini mchaichai, vitunguu (swaumu na maji), ulimi wa mama mkwe na marigold, inaweza kustawahi katika mazingira yote. Mimea hii inatajwa kuwa na uwezo wa kufukuza nyoka kutokana na harufu kali inayomkosesha raha nyoka, hivyo kumfanya asisogee kwenye eneo au bustani yako. MARIGOLD Wataalamu wanaeleza kuwa harufu yake na mizizi ya marigold huwafukuza nyoka. Mkulima katika kijiji cha Onana,…

Read More

Na Restuta James SERIKALI imetangaza neema ya ufadhili wa masomo kwa vijana 8,000, ambao watagharimiwa kwa asilimia 100 kusomea ufundi stadi wa aina mbalimbali. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), juzi ilieleza kuwa ufadhili huo ni ruzuku ambayo walengwa hawatarudisha kama inavyofanyika kwa wanaojiunga vyuo vikuu nchini. Taarifa hiyo ilieleza kuwa vijana wanaopaswa kuomba ufadhili huo ni wenye umri wa miaka 15 hadi 35; na yatatolewa chini ya programu ya kukuza ujuzi nchini, inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki, ili kumudu ushindani katika soko…

Read More

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam MAENDELEO benki imeendeleza historia yake ya kupata faida kwa miaka 10 mfululizo, kwa kupata faida ya Sh. bilioni 3.69 kabla ya kodi mwaka jana 2024, ukilinganisha na Sh. bilioni 2.63, mwaka juzi 2023. Aidha, ongezeko hilo ni sawa na ukuaji wa asilimia 40, wakati faida baada ya kodi Sh. bilioni 2.83 na mapato halisi yatokanayo na riba yakiwa Sh. bilioni 10.84 ukilinganisha na Sh. bilioni 8.05 sawa na ukuaji wa asilimia 35, huku uwiano wa gharama kwa mapato ikifikia asilimia 61. Akizungumza na waandishi wa habari Februari 03, 2025, mkoani Dar es Salaam, Mkuu…

Read More

Taasisi za serikali na vyuo vikuu, zimetangaza mkakati wa kuwafaidisha wabunifu na watafiti, kutumia kazi zao kibiashara na kujipatia maendeleo, badala ya kazi zao kuishi kwenye makabati. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. William Anangisye, aliyasema hayo juzi Novemba 04, 2024 jijini Dar es Salaam na kutoa rai kwa wabunifu kuchangamkia utajiri uliopo kwenye miliki ubunifu (IP), alipokuwa akifungua mafunzo ya wataalamu mbalimbali kuhusu eneo hilo. Alisema uwekezaji na viwanda, vinategemea ubunifu na utafiti ili kuzalisha bidhaa mpya au kuboresha zilizopo na kutatua changamoto zinazoikabili jamii. “Watu wanafanya utafiti unaishia kwenye makabati tu, lakini sasa…

Read More

Sekta za kilimo, uvuvi na mifugo, zinafanyiwa utafiti wa kina, ili zitumike kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa yanayolenga kumaliza njaa ifikapo mwaka 2030. Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi, Anna Makinda, ameyasema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya siku 14 kwa wadadisi na wasimamizi 178 wa kilimo kwa mwaka wa 2023/2024, yaliyofanyika katika Chuo cha Afya ya Msingi, mjini Iringa. Amesema jukumu la wadadisi na wasimamizi hao litakuwa ni kukusanya na kuchambua takwimu sahihi za uzalishaji katika sekta hizo. “Roho na uhai wa nchi unategemea takwimu sahihi. Takwimu hizi zitawasaidia wakulima kujua ni kiasi gani cha…

Read More

CHANGAMOTO ya kupanga bajeti, kuweka akiba, uwekezaji, mikopo, bima na mipango mingine ya kifedha, sasa imepatiwa ufumbuzi baada ya benki ya NMB kuanzisha mpango mahsusi wa kutoa elimu endelevu ya kifedha. Akizindua NMB Nondo za Pesa mapema wiki hii, Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Filbert Mponzi, alisema walengwa wa programu hiyo ni Watanzania wote, lakini kwa upekee, itakuwa na vipengele maalumu vinavyowagusa vijana na wanawake. Mponzi, ambaye alimwakilisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema kupitia Nondo za Pesa, benki yake itakuwa inatoa elimu kwenye mada muhimu zote kuhusiana na fedha, ikiwamo namna ya…

Read More

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kituo cha Tengeru kimeanza kuzalisha miche 100,000 ya parachichi aina ya HASS, ambayo itauzwa kwa wakulima kwa bei elekezi. Taarifa iliyotolewa na TARI kwa umma kupitia mitandao yake ya kijamii leo, imeeleza kuwa miche hiyo itakuwa bora na taasisi hiyo itaifikisha kwa wakulima katika msimu ujao wa kilimo kupitia ofisi za halmashauri. DONDOO MUHIMU KUHUSU HASS Watafiti wameeleza kuwa, Hass ni miparachichi inayozaa mapema kuanzia miaka miwili na nusu hadi mitatu tangu kupandwa na haina magonjwa na wadudu kutokana na uandaji bora. Sifa nyingine ni vikonyo vya kubebeshea huchukuliwa kwenye miti halisi ya…

Read More

Shilingi 2.2 bilioni zilizowekezwa kwenye katika mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT- Mifugo na Uvuvi), zimeanza kuzaa matunda baada vijana kupata faida kutokana na uvuvi wa vizimba. Kikundi cha wajasiriamali wa uvuvi wa samaki kwa kutumia vizimba kinachoitwa Twihame, cha jijini Mwanza kimefanikiwa kuvuna zaidi ya samaki 4,000 katika kizimba kimoja wenye thamani ya Sh. 30 milioni. Kwa upande wake, kikundi cha Nguvu Kazi kimefanikiwa kupata zaidi ya Sh. 100 milioni, baada ya Septemba mwaka huu, kuvuna samaki waliowafuga kwa njia ya vizimba. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amevipongeza vikundi hivyo sambamba na kumshukuru Rais Samia kwa…

Read More

Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), limetenga dola za nchi hiyo milioni 24 (Sh. 60 bilioni), kwa ajili kupunguza upotevu wa chakula baada ya mavuno. Fedha hizo zinalenga kuimarisha usalama wa chakula, kupitia mradi wa Feed the Future Tanzania -Tuhifadhi Chakula. Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za ubalozi huo, zinaeleza kuwa mradi huo utatekelezwa kwa miaka mitano; na unalenga kupunguza upotevu wa chakula baada ya mavuno katika minyororo ya thamani ya kilimo cha mboga mboga na nafaka nchini. Mradi utatekelezwa na Chama cha Kilimo cha Mboga Mboga Tanzania (TAHA) na Mpango…

Read More