WANANCHI 75,000 wamefikiwa na programu ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA), katika mikoa nane, wengi wao wakiwa ni wanawake na vijana.
Akizungumza na BUSTANI jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, amesema lengo la mpango huo ni kuimarisha uchumi wa vijana, wanawake, watu wenye ulemavu pamoja na wazee, ambao tayari wanafanya biashara ndogo ndogo kwenye vikundi au mmoja mmoja.
“Tumelenga kufikia nchi nzima, tutakwenda mikoa yote Bara na Zanzibar…tumeshaenda mikoa nane na sasa tunakwenda mikoa mitano. Nia kubwa ni kutengeneza kanzi data ili tujue shughuli wanazofanya, mitaji, mapungufu waliyonayo na vile walivyonavyo ili tujue vipaumbele vya kila mkoa,” amesema.
Amesema baada ya kupita mikoa yote, serikali itafanya tathmini ili itengeneze programu itakayosaidia kundi kubwa la wananchi kujikwamua kiuchumi.
Amesema tathmini ya sasa inaonyesha kwamba kipaumbele cha kukuza uchumi wa wananchi wengi ni kilimo.
Baadhi ya mikoa ambayo imefikiwa na mpango wa IMASA ni Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Ruvuma na Dodoma.
Trending
- BRELA, UDSM wawanoa wadau faida miliki ubunifu
- Utafiti kilimo, mifugo na uvuvi kutokomeza njaa
- NMB yaja na mwarobaini mikopo kausha damu
- TARI kuzalisha miche 100,000 ya parachichi msimu ujao
- BBT YAANZA KUZAA MATUNDA KWENYE UVUVI
- MAREKANI YATOA BIL 60/- KUIMARISHA USALAMA WA CHAKULA
- BOT YAONYA APP ZA MIKOPO MTANDAONI, YAPIGA MARUFUKU UDHALILISHAJI
- VIJANA, WANAWAKE WAPEWA MITAJI WEZESHI MILIONI 101/-