Na Restuta James
FAMILIA nyingi kama sio zote zenye uwezo wa kununua televisheni au radio wanazo. Nyumba hizo hizo, ni chache au chini ya nusu hazina maktaba walau ya vitabu vichache.
Hali hii imejenga tabia ya wanafamilia na hasa watoto kupenda kuangalia na kusikiliza vipindi zaidi badala ya kusoma.
Kama wewe ni mzazi au mlezi nakuletea mbinu ya kuanzisha maktaba ndogo nyumbani ili watoto wanufaike na maarifa mengi yaliyofichwa vitabuni.
Walimu wa watoto wadogo wanaeleza kuwa mtoto mwenye umri kuanzia miaka miwili na nusu wanauwezo wa kujifunza kusoma na wakajua ndani ya muda mfupi, kama mazingira wenzeshi wataanzia nyumbani.
Wanashauri kuwa ni wajibu wa mzazi/mlezi kujenga tabia ya kujisomea nyumbani.
• Tengeneza shelvu la kuvutia
• Tenga muda wa kusoma pamoja
• Mpe mtoto muda wa kuzijua herufi, anaposhindwa kwenda kwa kasi unayoitaka usimwadhibu
• Usisome tu, chora pia
Kwa wenye nyumba kubwa, tenga chumba kikubwa kwa ajili ya maktaba, kwa wenye nyumba ndogo tengeneza shelvu za ukutani kama zinavyoonekana pichani au kwa jinsi utakavyoona inafaa.