Na Restuta James
MWISHONI wa juma yaani Jumapili kulikuwa na vibe la aina yake baada ya kuhitimisha msimu wa ligi kuu ya Uingereza kwenye mchuano mkali kati ya klabu za Arsenal na Manchester City, zilizokuwa zikiwania taji la EPL lililotwaliwa na wenyeji wa Etihad waliochukua ‘ndoo’ kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya washika bunduki, Arsenal.
Ni hitimisho la aina yake hasa kutokana na kwamba mshindi wa taji alitarajiwa kutangazwa katika mechi ya 38 ya kufunga msimu; hivyo lilikumbwa na msongo wa kila aina. Katika mazingira hayo, ni vizuri ukawa na vitu vya kuimarisha afya yako kujiondoa kwenye msongo wa mawazo wa soka. Saladi ya matunda ni jawabu mujarabu.
Nikupe mbinu kadhaa za kutengeneza saladi ya matunda siyo tu kwa sababu ya kuhitimisha ligi bali kujenga afya ya familia kwa ujumla.
Ni kawaida kwenye familia nyingi kula aina moja ya tunda tena kipande pekee, lakini siyo vibaya siku moja moja tukaandaa mchanganyiko wenye aina tofauti za matunda.
Hivi sasa kuna upatikanaji wa parachichi kwa wingi, machungwa, mananasi, ndizi mbivu na matango; japokuwa unaweza kuandaa kwa kutumia matunda zaidi ya hayo niliyotaja yakiwamo zabibu, kiwi, papai, chenza, embe na tikiti maji. Unaweza pia kutengeneza mishikaki ya matunda mchanganyiko.
DONDOO MUHIMU
Chukua matunda yako na utakate saizi unayoitaka, kila tunda liweke kwenye sehemu yake peke yake katika sinia. Salad nzuri inapendeza ukiweka vitunguu maji.
ZINGATIA: Unaweza kuweka mayai ya kuchemsha, nyanya na mahindi mabichi yaliyochemshwa kulingana na namna ulivyokata matunda.