WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wamesaini makubaliano na Taasisi nne za Serikali ya kushirikiana ili kuleta ufanisi katika maeneo mbalimbali ya kibiashara.
BRELA na Chuo Kikuu Mzumbe, TIA na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viutilifu Tanzania (TPHPA), wamesaini makubaliano hayo, leo Mei 9, 2024 kwenye maadhimisho ya siku ya Miliki Ubunifu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji, ameiagiza BRELA na COSOTA kutoa elimu zaidi kwa wabunifu nchini ili wanufuike na kazi zao na kuhakikisha inatambulika, ili wabunifu waweze kukopesheka na kuendeleza kazi zao.
“BRELA na COSOTA angalieni namna ya kutoa elimu ya miliki ubunifu kwa wabunifu wakiwamo wasanii wachanga, ili wanufaike na kazi zao,” amesema Mwinjuma.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa, amesema elimu ya Miliki Ubunifu bado iko chini na kwamba taasisi yake itaendelea kutoa elimu zaidi.
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha wanafikia malengo yao, wamekuwa na utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wafanyakazi wao kujiendeleza na masomo katika fani ya miliki bunifu ndani na nje ya nchi.
Katika hatua nyingine, Afisa Mtendaji Mkuu huyo na Naibu Waziri Mwinjuma, walikabidhi mfano wa hundi wa Sh. Million 16.5 kwa kila mmoja, wanufaika wanne wa masomo ya Miliki Ubunifu.
Trending
- BRELA, UDSM wawanoa wadau faida miliki ubunifu
- Utafiti kilimo, mifugo na uvuvi kutokomeza njaa
- NMB yaja na mwarobaini mikopo kausha damu
- TARI kuzalisha miche 100,000 ya parachichi msimu ujao
- BBT YAANZA KUZAA MATUNDA KWENYE UVUVI
- MAREKANI YATOA BIL 60/- KUIMARISHA USALAMA WA CHAKULA
- BOT YAONYA APP ZA MIKOPO MTANDAONI, YAPIGA MARUFUKU UDHALILISHAJI
- VIJANA, WANAWAKE WAPEWA MITAJI WEZESHI MILIONI 101/-