Na Mwandishi Wetu
DUNIA ya sayansi, teknolojia, ubunifu na uvumbuzi imeendelea kuleta mageuzi kwenye sekta ya majenzi na mapambo ya nyumba, ikiongeza vitu vipya kila siku.
Moja ya mambo yaliyoongezeka ni kusambaa kwa taarifa za kila kinachofanyika sehemu mbalimbali na hivyo kurahisisha upatikanaji wa maarifa kuhusu jambo lolote, ukiwa sehemu yoyote na hii ndiyo inayodhihirisha kwamba dunia ni kijiji.
Katika miaka ya karibuni, kwenye maduka mbalimbali mitandaoni, baadhi ya wabunifu wa samani wametengeneza zinazoitwa ‘zisizo za kawaida’ ambazo zimebuniwa kama picha za wanyama au ndege wakiwamo wa kutisha.
Kwenye mitandao zimeonyeshwa samani zilizobuniwa kama tembo, simba, chui, fisi, nguruwe, mbwa, farasi, paka, sokwe na nyoka; huku nyingine zikionekana kama bundi, tai, tausi na mbuni.
Ziko pia zinazotengenezwa kwa mwonekano wa vifaa kama gitaa, kinanda, gari ya kifahari au muundo wa kiatu kizuri.
Katika samani hizo, zipo meza za chakula, kahawa, sehemu ya jiko na sofa za ndani na nje ya nyumba kwenye bustani au kibarazani.
“Kinachofanya ziitwe zisizo za kawaida ni kwa sababu baadhi zinatisha sana, kwa mfano utakuta kiti kimetengenezwa kama chatu aliyejiviringisha na sehemu ya kujiegamiza ni mdomo wake. Kingine unakuta ni bundi au simba anayenguruma,” anafafanua fundi seremala Aloyce Michael.
Anasema ni watu wachache wanaopendelea samani za kutisha na kwamba badala yake wengi wanapendelea zaidi za wanyama wapole kama tembo kutokana na tabia za wanyama wengine kama mbwa.
Trending
- BRELA, UDSM wawanoa wadau faida miliki ubunifu
- Utafiti kilimo, mifugo na uvuvi kutokomeza njaa
- NMB yaja na mwarobaini mikopo kausha damu
- TARI kuzalisha miche 100,000 ya parachichi msimu ujao
- BBT YAANZA KUZAA MATUNDA KWENYE UVUVI
- MAREKANI YATOA BIL 60/- KUIMARISHA USALAMA WA CHAKULA
- BOT YAONYA APP ZA MIKOPO MTANDAONI, YAPIGA MARUFUKU UDHALILISHAJI
- VIJANA, WANAWAKE WAPEWA MITAJI WEZESHI MILIONI 101/-