Na Restuta James
NGULI wa nyimbo za injili nchini, Christina Shusho, amesema ‘kituo kinachofuata’ ni tamasha na maonesho ya biashara nchini Dubai, ambayo yatakwenda sambamba na mahubiri ya neno la Mungu.
Shusho ameiambia GND jijini Dar es Salaam jana alipokutana na wadau wa maandalizi wa safari ya Dubai kwa wapendwa wanaomiliki biashara.
Alisema safari hiyo imeandaliwa na Neema Ministry ya mtumishi wa Mungu, Nabii Neema Sikatenda, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Alisema safari ya Dubai inajumuisha matukio matano ambayo ni mikutano ya kibiashara, mikutano ya injili, onesho la muziki wa injili, utalii na maonesho ya kibiashara.
“Ni tukio muhimu kwa ajili ya kupata fursa za kibiashara, wabia, kukutana na watumishi wa Mungu wenye
karama tofauti, wana muziki wa injili wa kimataifa na utalii,” alisema.
Alisema nia ni kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wa nchi nyingine, ili waweze kuona fursa zilizopo ‘duniani’ na kueleza zile zinazopatikana Tanzania.
“Ni tamasha la kipekee linalotengeneza chanzo cha watu kukutana na kubadilishana uzoefu. Tutakutana kule kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 3, 2023,” alisema.
Shusho ambaye ni balozi wa huduma ya Neema Ministry, alisema kabla ya safari ya Dubai, mtumishi huyo anatarajiwa kufanya mkutano wa injili jijini Dar es Salaam.
Alisema akiwa Dar es Salaam, Sikatenda atakuwa na mikutano ya injili pamoja na ya kibiashara ambayo inalenga kuibua fursa zilizopo Afrika na nje ya bara hili.
Trending
- BRELA, UDSM wawanoa wadau faida miliki ubunifu
- Utafiti kilimo, mifugo na uvuvi kutokomeza njaa
- NMB yaja na mwarobaini mikopo kausha damu
- TARI kuzalisha miche 100,000 ya parachichi msimu ujao
- BBT YAANZA KUZAA MATUNDA KWENYE UVUVI
- MAREKANI YATOA BIL 60/- KUIMARISHA USALAMA WA CHAKULA
- BOT YAONYA APP ZA MIKOPO MTANDAONI, YAPIGA MARUFUKU UDHALILISHAJI
- VIJANA, WANAWAKE WAPEWA MITAJI WEZESHI MILIONI 101/-