Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), limetenga dola za nchi hiyo milioni 24 (Sh. 60 bilioni), kwa ajili kupunguza upotevu wa chakula baada ya mavuno.
Fedha hizo zinalenga kuimarisha usalama wa chakula, kupitia mradi wa Feed the Future Tanzania -Tuhifadhi Chakula.
Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za ubalozi huo, zinaeleza kuwa mradi huo utatekelezwa kwa miaka mitano; na unalenga kupunguza upotevu wa chakula baada ya mavuno katika minyororo ya thamani ya kilimo cha mboga mboga na nafaka nchini.
Mradi utatekelezwa na Chama cha Kilimo cha Mboga Mboga Tanzania (TAHA) na Mpango wa Kuboresha Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT).
Trending
- EPUKA MAUA HAYA NYUMBANI KWAKO
- FUKUZA NYOKA KWA MIMEA HII
- DARASA LA SABA KUPEWA UFADHILI
- MAENDELEO BENKI YATAJA ONGEZEKO LA FAIDA 2024
- BRELA, UDSM wawanoa wadau faida miliki ubunifu
- Utafiti kilimo, mifugo na uvuvi kutokomeza njaa
- NMB yaja na mwarobaini mikopo kausha damu
- TARI kuzalisha miche 100,000 ya parachichi msimu ujao