Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema itaendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa wakulima ili waweze kupata mikopo kwa riba nafuu itakayowasaidia kufikia malengo na kupiga hatua ya maendeleo.
Akizungumza kwenye mahojiano katika Maonesho ya kimataifa ya kilimo Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma, Afisa Mkuu Mwandamizi, Kurugenzi ya Usimamizi Sekta ya Fedha, Idara ya huduma ndogo ya Fedha, BoT, Deogratius Mnyamani, amesema BoT imetenga fedha kwa ajili ya taasisi za fedha zikiwamo benki ili waweze kuwakopesha wakuilimo kwa riba nafuu.
Amesema lengo ni kuhakikisha wakulima wanapata mikopo kwa gharama nafuu ili kuleta tija kwa Taifa katika sekta ya kilimo.
Amesema ili mkulima apige hatua anatakiwa kuongeza uwekezaji na kwamba taasisi za fedha zinapaswa kutoa mikopo kwa wakulima kwa kuzingatia riba nafuu ili kuhakikisha malengo yanafikiwa.
“Pia kuna fursa mbalimbali kwa wale ambao wanataka kuanzisha biashara za huduma za fedha katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini kwa kuwakopesha wakulima wadogo,”