Na Restuta James
KWA wapenda maua neno hydroponics haliwezi kuwa geni kwao kwa kuwa ni lugha ya mkitaalamu kwa mimea inayokua ndani ya maji pasipokuweka udogo.
Upandaji huu wa maua ni mzuri hasa kwa ‘walevi’ wa mimea kwani ni rahisi kuiweka popote ikiwamo jikoni, chumbani au chooni (kwa maua yanayosafisha hewa).
Upandaji huu wa mimea au maua haya una ‘ladha’ ya pekee ndani ya nyumba kutokana na kwamba yanatumia zaidi majagi ya udongo.
Wataalam wa bustani wanaeleza kuwa upandaji huu unavutia na kuongeza ‘usafi’ ndani ya nyumba kwa kuwa ua na chombo vyote ni lazima viwe visafi wakati wote.
Wanaeleza kuwa ubunifu unaweza kumsaidia mpenzi wa mimea kuanzisha bustani ya viungo au mimea tiba kama rosemary jikoni na kumfanya kupata hewa nzuri na kiungo kisicho na kemikali.
Wanashauri kwamba sehemu nzuri ya kuweka maua haya ni kona yoyote ya nyumba, kwenye ‘console’, meza ya chakula na meza ya vipodozi.
Kwa watu wa saluni, upandaji huu unaongeza thamani na kuwavutia wateja kwani maua au rangi ya ukijani inatajwa kutuliza sana akili.
Aidha, siyo maua tu ambayo unaweza kupanda kwenye maji, zipo pia aina mbalimbali za mboga unazoweza kuziotesha ndani mwako na ukafurahia mlo mzuri kila siku.
DONDOO MUHIMU
• Ni lazima ukumbuke kubadilisha maji kila wiki au walau kila baada ya wiki mbili. Katika hili, hakikisha unatenga siku yako ya mapumziko kuwa ndiyo ya kubadiliisha pia maji ya mimea yako.
• Hakikisha ua au mimea yako unaiweka karibu na dirisha ili iweze kupata jua na kupata afya nzuri.
• Maua haya yanawekwa kwenye orodha ya usafi na umaridadi usiokifani.
• Bustani nzuri kwa wavivu wa bustani.
Trending
- BRELA, UDSM wawanoa wadau faida miliki ubunifu
- Utafiti kilimo, mifugo na uvuvi kutokomeza njaa
- NMB yaja na mwarobaini mikopo kausha damu
- TARI kuzalisha miche 100,000 ya parachichi msimu ujao
- BBT YAANZA KUZAA MATUNDA KWENYE UVUVI
- MAREKANI YATOA BIL 60/- KUIMARISHA USALAMA WA CHAKULA
- BOT YAONYA APP ZA MIKOPO MTANDAONI, YAPIGA MARUFUKU UDHALILISHAJI
- VIJANA, WANAWAKE WAPEWA MITAJI WEZESHI MILIONI 101/-