
TAASISI ya Saratani Ocean Road (ORCI), imetenga siku maalumu ya uchunguzi wa saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino.
Taarifa ya ORCI iliyotolewa leo imesema kwamba taasisi hiyo imetenga saa saba kila siku ya Alhamisi kuhudumia kundi hilo la wagonjwa.
“Kliniki ya saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino kila Alhamisi kuanzia saa 2:00 hadi saa 9:00 alasiri block A-chumba namba 110,” imesema.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa: “Karibu upate elimu na uchunguzi wa awali wa saratani…karibuni hata kwa watu wengine wa kawaida.”