TAASISI ya Afya Ifakara (IHI), imeanza kampeni kubwa ya chanjo ya mbwa ili kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Kampeni hiyo inafanyika kwa siku 10, kuanzia Jumamosi iliyopita hadi kesho Jumatano.
Akizungumza na NIPASHE, kiongozi wa kampeni hiyo kutoka IHI, Dk. Sambo Maganga, amesema kampeni hiyo inafanyika Manispaa ya Tabora Mjini na wanatarajia kuchanja mbwa 15,000 ili kudhibiti ugonjwa huo katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taasisi hiyo, ugonjwa wa kichaa cha mbwa husababisha vifo vya watu 552 nchini kwa mwaka huku asilimia 98 waking’atwa na mbwa wa kufugwa.
Trending
- EPUKA MAUA HAYA NYUMBANI KWAKO
- FUKUZA NYOKA KWA MIMEA HII
- DARASA LA SABA KUPEWA UFADHILI
- MAENDELEO BENKI YATAJA ONGEZEKO LA FAIDA 2024
- BRELA, UDSM wawanoa wadau faida miliki ubunifu
- Utafiti kilimo, mifugo na uvuvi kutokomeza njaa
- NMB yaja na mwarobaini mikopo kausha damu
- TARI kuzalisha miche 100,000 ya parachichi msimu ujao