Mwandishi Wetu na Mtandao
KUNA watu ambao huwezi kukadiria umri wao licha ya kwamba wana miaka mingi, mwonekano wao unabakia kuwa wa ujana.
Orodha ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), inawataja nyota kadhaa wa muziki na filamu, ambao kwa miaka mingi wamesalia kama walivyokua walipojitosa katika fani ya burudani.
Kuanzia Afrika, orodha ya BBC inamtaja mwigizaji wa Nollywood nchini Nigeria, Kate Henshaw (51), ambaye mwonekano wake haufanani na miaka aliyonayo.
Mashabiki wengi wa Kate walikadiria ana miaka 30, wakati aliposherehekea miaka 50 tangu kuzaliwa kwake.
Kwa ufupi ni kwamba Kate Henshaw aliolewa na raia wa Uingereza, Roderick James Nuttal, mwaka wa 1999 na wakajaaliwa mtoto wa kike mnamo mwaka wa 2000. Hata hivyo ndoa yao ya miaka 12 iliisha na kila mtu akashika njia yake.
Kate anataja siri ya yeye kubakia na urembo wake ni kudensi na kufanya mazoezi.
Kate ameshinda tuzo nyingi za filamu na kushirikishwa katika filamu nyingi za Nigeria zikiwemo “When the Sun Set’ ‘Chief Daddy’, ‘The Wives’, ‘Games Men Play’, ‘Scars of Womanhood’ na ‘Roti.’
WILL SMITH
Mwanzoni mwa milenia, Will Smith (54), alikuwa na miaka 21. Hata hivyo, mwonekano wake hauendani na umri wake na kwa watoto waliozaliwa mwaka 20 iliyopita wanaweza kudhani Smith ni ‘mwenzao.’
J. LO
Jennifer Lopez (53), anaoneka kama alivyokuwa miaka 20 iliyopita licha ya kwamba ameshakaa miongo mitano duniani.
Urembo na mvuto wake unaomfanya aonekane bado mdogo kiasi cha kupewa jina la ‘J. Glow’
Mbali na kuwa na ratiba ngumu ya maigizo, kutengeneza muziki, kutumbuiza kwenye matamasha na kwenda kwenye uzinduzi wa filamu mbalimbali, kufanya mazoezi na kulea watoto wake wawili, Max na Emme, Lopez anasema hupata muda wa kupata usingizi wa kutosha.
Kunywa maji mengi, kula vyakula halisi, matunda mengi na mboga za majani ninakuwa navyo wakati wote, vyote vina nafasi katika muonekano wa ngozi yangu,” anaeleza J.Lo.
BEYONCE
Mwaka 2003, Beyonce alikuwa na miaka 22 na leo ana miaka 42 lakini bado anaonekana kama kijana anayekaribia miaka 30.
Kutoka Destiny’s Child hadi mshindi wa tuzo za Grammy, mwanamuziki wa kujitegemea na mama wa watoto watatu- Blue, Sir na Rumi; bado yu mrembo pamoja na umri wake kusonga.
JACQUELINE MENGI
Mbali ya orodha hiyo ya BBC, Mtandao wa GND unataja orodha ya nyota wa Tanzania wasiozeeka wakianza na mlimbwende Jackline Ntuyabaliwe Mengi.
Jackline mama wa watoto wawili, Jaydane na Ryan, ambao ni mapacha.
FLAVIAN MATATA
Flaviana Matata (35), ni malkia wa urembo na mwanamitindo wa kimataifa akitokea Miss Universe aliposhinda taji la mashindano hayo mwaka 2007.
Ni miongoni mwa wanamitindo saba waliorekodiwa kuwa na mapato ya juu zaidi barani Afrika akitajwa na Forbes Afrika mwaka 2013.
Mwaka 2017 alitajwa na okay.com kuwa mmoja wa wanawake 100 wenye ushawishi Afrika.
Ngozi yake na mwili wake ni vitu vinavyomuweka kwenye ujana kila siku licha ya umri wake kuendelea kusogea.